Athari 5 za pombe kwenye mwili wako

HomeElimu

Athari 5 za pombe kwenye mwili wako

Tambua kwamba unapaswa kuangalia tabia zako za unywaji pombe kwani ukinywa wastani ina faida kwa mwili wako lakini mwili unaumizwa na kuharibikiwa endapo utakuwa ni mnywaji pombe kupita kiasi.

Hizi hapa baadhi ya madhara ya pombe kupita kiasi:

1. Kushuka kwa kinga ya mwili
Hunywaji pombe kupita kiasi huchukua chembechembe za nyeupe ambazo zinahusika na kupigana na magonjwa na kuzifanya kushindwa kufanya kazi kikamilifu na hii hupelekea mtu kushambuliwa na magonjwa tofauti mara kwa mara.

2. Pombe husababisha utapiamlo
Pombe huathiri bakteria kwenye matumbo yetu yetu ambao wanahusika na kuvunja chakula. Unywaji wa pombe kupita kiasi husababisha matatizo mengi ya usagaji wa chakula, vidonda vya tumbo, kutokwa na damu ndani, ugonjwa wa fizi na kuoza kwa meno.

3. Pombe huathiri kazi ya ubongo na kupoteza kumbukumbu
Unywaji pombe kupita kiasi kunaweza kusababisha kupunguza nguvu na kasi ya ubongo kufanya kazi ipasavyo, na ndio maana mlevi anapoongea huwa haeleweki na wakati mwingine hawezi kukumbuka chochote.

4. Pombe huathiri uzazi
Unywaji pombe kupita kiasi unaweza kusababisha tatizo la nguvu za kiume kwa wanaume na kuathiri uzalishaji wa baadhi ya homoni kwa wanawake jambo ambalo baadae husababisha matatizo ya uzazi.

5. Unywaji pombe huathiri ini
Pombe kupita kiasi husababisha kongosho kusitisha utengenezaji wa insulini. Pia husabisha ini kushindwa kufanya kazi vizuri na kuzalisha tatizo la homa ya ini, homa ya manjano na ugonjwa wa cirrhosis.

error: Content is protected !!