Atupa lawama kwa bodi

HomeMichezo

Atupa lawama kwa bodi

Mmiliki wa klabu ya Simba, Mohamed Dewji ametupia lawama kwa bodi ya timu hiyo baada ya kupoteza mchezo wa nusu fainali dhidi ya Yanga leo Mei 28, 2022 Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Katika ujumbe wake Mo Dewji ameandika bodi inapaswa kuchukua hatua kali na zaharaka zaidi ili kuweza kuhakikisha wanarudi katika mstari.

Yanga imetinga Fainali ya Kombe la Azam Sports Federation CuP (ASFC) kwa kuwatwanga watani zao Simba 1-0 leo katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Bao hilo pekee limefungwa kwa shuti kali nje ya 18 na Feisal Salum ‘Fei Toto’ dakika 25 na kuwavua ubingwa huo iliyokuwa inautetea.

error: Content is protected !!