Aweso amuwakilisha Rais Samia Mkutano wa UN

HomeKitaifa

Aweso amuwakilisha Rais Samia Mkutano wa UN

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Hamidu Aweso anamwakilisha Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Maji unaofanyika Umoja wa Mataifa, New York, tarehe 22-24 Machi 2023.

Waziri Aweso amehutubia Mkutano huo jana jioni ambapo Katika hotuba yake amebainisha umuhimu wa dunia kukaa pamoja na kusimamia agenda ya maji; thamani ya maji katika maisha na uchumi; kuongeza uwekezaji katika eneo la maji; ushirikiano wa kimataifa katika maji; pamoja na utafutaji wa fedha kwa ajili ya maji.

Aidha, Katika mkutano, Tanzania imebeba agenda mbili ambazo ni utekelezaji wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji Awamu ya Tatu (Water Sector Development Programe III) ambayo inahitaji Dola za Marekani Bilioni 6.47 katika kipindi cha 2022-2025.

Vilevile, Tanzania imejipambanua kwa agenda ya uwekezaji katika Sekta ya Maji ili kufikia Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (Tanzania Water Investment Programme 2023-2030). Programme ambayo bado inaandaliwa na ipo hatua za mwisho kuzinduliwa inakadiriwa kuwa na bajeti ya zaidi ya Dola za Kimarekani Bilioni 25 na itazinduliwa Mei 2023.

error: Content is protected !!