Baada ya miaka 10, chanjo ya kwanza ya Malaria yathibitishwa

HomeElimu

Baada ya miaka 10, chanjo ya kwanza ya Malaria yathibitishwa

Malaria ni ugonjwa unaosababishwa na vilemea aina nne: P falciparum, P Malarie, P. Ovale na P. vivax. Vimelea hivyo hubebwa na kusambazwa na mbu jike wanaojulikana kama Anapheles pindi wamuumapo binadamu.

Kitengo cha Afya Umoja wa Mataifa (UN) kimethibitisha matumizi ya chanjo ya ‘Mosquirix’ ambayo ni chanjo dhidi ya ugonjwa hatari wa malaria kwa watoto barani Afrika.

Ugonjwa wa Malaria huua mtoto mmoja kila baada ya dakika mbili huku visa vipya zaidi ya milioni 200 vikiripotiwa kila mwaka, hii ni kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).

Kukabiliana na janga hilo, WHO imethibitisha chanjo ambayo inakuwa chanjo ya kwanza kuthibitishwa katika historia ya majaribio ya chanjo za ugonjwa wa Malaria. Majaribio na utafiti wa chanjo hiyo yamechukua miaka 10 na yamefanyika ndani ya nchi saba.

“Chanjo tuliyoingoja kwa miaka mingi imefika, ni mafanikio makubwa sana kwenye sayansi. Tunajivunia sana kwa kuwa chanjo hii imetengenezwa Afrika na wanasayansi wa kiafrika,” Tedros Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu Shirika la Afya Duniani (WHO) amesema.

   > Utafiti: Namna Vitamin A inavyoweza kutibu tatizo la UVIKO-19

Malaria huua watu wengi zaidi barani Afrika, ambapo kwa mujibu wa takwimu za WHO mwaka 2019 Malaria imeua watu 386,000 ikilinganisha na UVIKO-19 ambapo hadi sasa vifo vilivyothibitishwa ni 212,000 katika miezi 18 iliyopita. WHO inasema kuwa visa 94% vya Malaria kote duniani hutokea barani Afrika, bara lenye watu bilioni 1.3.

Chanjo ya Malaria imethibitishwa kuwa na uwezo wa 30% katika kuzuia visa vibaya vya Malaria dhidi ya watoto.

Fahamu haya kuhusu Malaria:

– Ni ugonjwa unaozuilika na kutibiwa pia
– Mwaka 2017, kuliripotiwa visa karibu milioni 219 vya ugonjwa wa Malaria katika nchi 87 kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO)
– Inakadiriwa kuwa watu 435,000 walifariki dunia kutoka na Malaria mwaka 2017
– Inakadiriwa kuwa karibu dola bilioni 3.1 zilitumika kudhibiti na kuangamiza malaria mwaka 2017

error: Content is protected !!