Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa tukio la mtoto wa miezi 11 kunajisiwa na baba yake wa kambo anayeishi eneo la Amboni jijini Tanga.
Kamanda Jongo alisema mtoto huyo alikuwa amebebwa mgongoni na mama yake huku baba yake kwa sababu michezo hiyo alikuwa ameizoea akawa anamnajisi ndipo mama yake alipomwona.
“Kwa hiyo baba huyo hatua za kisheria zinaendelea kwa lengo la kuhakikisha mtuhumiwa anachukuliwa hatua kali za kisheria ili kuwa fundisho kwa watu waenye tabia za namna hiyo,” alisema Kamanda Jongo.
Aidha, Kamanda Jongo amewaambia wananchi kuwa hato vumilia matukio ya namna hiyo kwenye mkoa wa Tanga hivyo sheria itachukuliwa kwa kila atakaye husika na matukio hayo.