Balozi wa Marekani nchini, Michael Battle ameisifia treni ya Reli ya Kisasa (SGR) kwa huduma bora na huku akisema amesafiri mabara manne duniani ila anajivunia huduma bora ya usafiri wa treni hiyo kwa Tanzania.
Kauli hiyo ametoa kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X jana alipoweja ujumbe huo na picha yake aliyopiga akiwa nje ya sehemu ya mabehewa ya treni hiyo.
Aliandika “Treni kutoka Dar kwenda Dodoma. Nimepanda treni kwenye mabara manne na ninajivunia kusema kuwa Tanzania inatoa uzoefu bora wa kipekee wa treni. Treni iliondoka stesheni kwa wakati, safari ilikuwa ya starehe, ukarimu na umahiri wa watoa huduma bora ndani ya treni”.
Pongezi hizo ni fahari kwa Watanzania kwa kazi nzuri inayoendelea kufanywa na serikali kupitia utekelezaji wa miradi ya kimkakati na maendeleo.