Bandari ya Mtwara yapeleka tani 15,800 za korosho Vietnam

HomeKitaifa

Bandari ya Mtwara yapeleka tani 15,800 za korosho Vietnam

Siku ya jana Juni 22, 2022 imekuwa ya neema kwa wakazi wa Mtwara na maeneo ya jirani kwa sababu Meli Iliyobeba Korosho Tani elf 15,800 imeondoka Katika Bandari ya Mtwara kuelekea Nchini Vietnam.

Kuondoka kwa meli hii iliyobeba tani elfu 15 za Korosho inafanya jumla ya Tani 51,200 za Korosho kusafirishwa kupitia Bandari ya Mtwara kwenda kwenye masoko ya nje.

Akiongea na wana habari Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania Brigedia Jenerali Mstaafu Aloyce Mwanjile Amesema

“Hatua hiyo inakuja kufuatia kampuni ya Sibatanza ya nchini Vietinam kununua Tani elfu 80 katika msimu ulioisha na tayari imesafirisha awamu mbili za korosho hivyo zilibaki Tani elf 15 tu ambazo Leo zimeondika”

Mbali na Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania Brigedia Jenerali Mstaafu Aloyce Mwanjile pia Kaimu Mkurugenzi Ndugu Francis Alfred amesema “ ujio wa Meli hizi umewahakikishia wakulima na taifa kwa ujumla soko la korosho la uhakika lakini pia kwa wananchi wa Mtwara na Mikoa mingine ya jirani”

error: Content is protected !!