Batu tale akemea ‘machawa’

HomeKitaifa

Batu tale akemea ‘machawa’

Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Hamisi Shaban Taletale maarufu Babu Tale ambaye pia ni meneja wa msanii Diamond Platnumz kutoka lebo ya Wasafi amewataja Mwijaku, Baba Levo na Juma Lokole kama wagombanishi wa wasanii na ndio chanzo cha matatizo yanayoendelea kati ya Harmonize na Diamond.

“Tuwapinge hawa wagombanishi wachache Mwijaku, Baba Levo huyu Juma Lokole hawa ndio wapumbavu, tuwatoe hawa kwenye industry yetu tusapoti muziki wetu tuwashawishi wasanii wafanye vizuri,” alisema Babu Tale.

Babu Tale aliwataka waandishi wa habari kuacha kutoa kipaumbele kwa watu wanaochochea ugomvi baina ya wasanii na kusema kuwa watu hao hawachangamshi muziki bali wanakuza bifu zisizoza msingi na kushusha thamani ya muziki wa Tanzania.

Pia amewataka wasanii na waandishi wa habari kutangaza Tanzania vizuri kwenye mitandao ya kijamii akitolea mfano jinsi alivyompa Maluma, gwiji wa muziki kutokea nchini Columbia kusoma maneno ya kiswahili yaliyoandikwa kwenye ukurasa wa Instagram wa Clouds.

error: Content is protected !!