Benard Morrison atakiwa kuirudishia Yanga fedha baada ya kushinda kesi

HomeUncategorized

Benard Morrison atakiwa kuirudishia Yanga fedha baada ya kushinda kesi

Mahakama ya usuluhishi wa kesi za michezo Duniani (CAS) imetupilia mbali rufaa ya timu ya soka Yanga ya kupinga uamuzi uliotolewa na kamati ya sheria na hadhi za wachezaji kwamba  mchezaji wa kimataifa wa Ghana Bernard Morrison hakuwa na mkataba nao kipindi anajiunga na timu ya soka Simba.

Agosti 2020, Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la mpira wa miguu hapa Tanzania (TFF) iliamua kwamba Benard Morrison alikuwa huru kujiunga na Simba kwani mkataba wake na Yake ulikuwa umemalizika, huku Yanga wakisisitiza kwamba Morrison alikubali kusajiliwa na Simba akiwa bado ni mchezaji wao halali.

Sakata hilo lilichukua muda mrefu baada ya CAS kuahirisha mara kwa mra kutoa huku ya Shauri hilo, na kufanya wapenzi wa soka nchini kote kusubiri hatma ya Benard Morrison. Kesi hiyo ilifanya Morrison apachikwe jina la utani la ‘wakili msomi’ kutokana na namna ambavyo alikuwa anakwenda Mahakamani mara kwa mara.

hat hivyo, CAS imethiboitisha kwamba Yanga ilimpatia Morrison fedha kiasi cha dola 30,000 za Kimarekani na hivyo Morrison ametakiwa kuirudishia Yanga fedha hizo.

error: Content is protected !!