Benki ya Dunia kushirikiana zaidi na Tanzania

HomeKitaifa

Benki ya Dunia kushirikiana zaidi na Tanzania

Benki ya Dunia iimesema itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kukuza uchumi kupitia mabadiliko ya kidijitali kwa kushirikiana na sekta binafsi.

Ahadi hiyo imetolewa na Rais wa Benki ya Dunia, David Malpass alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan nchini Marekani.

Mbali na hilo Malpass amempongeza Rais Samia kwa jitihada za kupambana na UVIKO 19 nchini Tanzania.

Kwa upande wake Rais Samia ameishukuru Benki ya Dunia kwa mchango wake kwa Tanzania katika huduma za jamii pamoja na mapambano dhidi ya UVIKO 19.

Vilevile, Rais Samia amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani (WTO), Bi. Ngozi Okonjo-Iweala ambapo viongozi hao wamezungumzia kuwezesha biashara kwa kuimarisha upatikanaji wa chanjo, usimamizi wa uvuvi na kilimo.

error: Content is protected !!