Bil 2.6 zalipwa na NSSF kwa vyeti feki

HomeKitaifa

Bil 2.6 zalipwa na NSSF kwa vyeti feki

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jmaii (NSSF) imetumia Sh bilioni 2.6 kuwalipa watumishi 183 waliofutiwa ajira kwa kukutwa na vyeti feki.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mfuko na mwelekeo wa watendaji katika mwaka wa fedha 2022/23.

Mshomba alisem akatika nusu ya mwaka wa fedha iliyoisha Desemba 2022, Mfuko ulilipa mafao ya Sh bilioni 350.7 kwa wanachama , wastaafu na wanufaika wengine wapatao 80,339.

“Malipo haya yanajumuisha Sh bilioni 2.6 zilizolipwa kwa watumishi 183 waliofutiwa ajira kwa kukosa vyeti halali.”

Hatua hiyo imechochewa na agizo la Rais Samia Suluhu la kulipwa fedha za michango waliochangia watumishi walioondolewa kazini kutokana na vyeti feki.

Aidha, Mshomba alisisitiza kwamba bado NSSF inaendelea kuwalipa watumishi wao lakini hatarajii idadi kuongezeka zaidi kutokana na mfuko huo kuwa na idadi ndogo ya watumishi wa umma waliokuwa wakichangia mfuko huo.

error: Content is protected !!