Namna ya kusherekea Valentine’s Day kama upo ‘singo’

HomeMakala

Namna ya kusherekea Valentine’s Day kama upo ‘singo’

Ikiwa inakaribia siku ya wapendanao tarehe 14 mwezi Februari, tayari mitandaoni watu wameanza kuonyesha shauku ya kusubiria siku hiyo huku wengi wao wakiwa wale waliopo kwenye mahusiano.

Siku hiyo watu hupeana zawadi mbalimbali kama maua, magari, simu, saa, nyumba na vitu vingine mbalimbali vinavyoashiria upendo kati yao, lakini je ambaye huna mahusiano umejiandaaje siku hiyo?

Ili usiwe mnyonge, ClickHabari tumefanikiwa kukuandalia baadhi ya mambo ambayo unaweza kufanya siku hiyo ili usijione mpweke.

Jinunulie zawadi kisha ichapishe mtandaoni
Usisubiri mpaka mtu akununulie zawadi. Huenda ukawa umeona kitu kizuri na ukatamani mtu akununulie lakini hayupo, usijali maana unachotakiwa kufanya ni kununua hiyo zawadi ifunge vizuri kisha ichapishwe kwenye mtandao wowote ukiandika “Kutoka kwa mpenzi wangu wa maisha”.

Badilishana zawadi na rafiki yako ambaye yupo ‘Singo’
Kama Valentine ni siku ya wapendanao basi isisherekewe tu na watu waliopo kwenye mahusiano. Hivyo basi unaweeza kununua zawadi ukampa rafiki yako ambaye hayupo kwenye mahusiano na yeye akakupa zawadi pia.

Jiambie kwamba wewe ni bora
Jiambie kwamba wewe ni bora kuliko mtu yeyote na huitaji kupendwa ndio utambulike kama wewe ni bora. Jiambie kwamba una muda mzuri na unaweza kufanya mambo makubwa yenye manufaa ukiwa haupo kwenye mahusiano sababu ukiwa na mtu anaweza kukupa msongo wa mawazo hivyo kushindwa kutimiza malengo yako.

Fanya kitu unachopenda
Itumie siku hii kufanya kitu unachopenda mfano kupika, kusikiliza muziki, kucheza mpira au hata kufanya mazoezi. Kufanya hivyo kutakufanya usiwe na mawazo kuhusu siku ya wapendao.

 

 

error: Content is protected !!