Bodaboda Arusha wamjibu Lema kuwaita ‘wakimbiza upepo’

HomeKitaifa

Bodaboda Arusha wamjibu Lema kuwaita ‘wakimbiza upepo’

Uongozi wa Umoja wa Bodaboda wilayani Arusha (UBOJA) wamelaani kauli iliyotolewa na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini  (Chadema), Godbless Lema kwamba biashara ya kuendesha pikipiki siyo kazi bali ni kazi ya kukimbiza upepo.

Akizungumza kauli hiyo, Katibu wa UBOJA, Hakimu  Msemo, alisema kauli iliyotolewa katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Relini jijini Arusha, juzi ni kauli ya kejeli ambayo imewaudhi waendesha pikipiki.

“Tumepokea kwa masikitiko makubwa kauli iliyotolewa na Lema dhidi ya bodaboda kwamba tunafanya kazi ua kukimbiza upepo wakati ni kazi ambayo ina manufaa kwetu, kauli hiyo ya kejeli imetukera na hatutampatia ushirikiano kwa sababu hana nia njema dhidi ya waendesha bodaboda wa jiji la Arusha.

Aliongeza kuwa : “Tunamtaka Lema atambue kuwa Arusha kuna vijana waendesha bodaboda zaidi ya elfu 12 na wote wanajipaia kipato chao, wengine wamejenga, wanasomesha watoto na kulisha familia kwa kazi hiyo. Anapozungumza atambue kuwa anazungumzia ajira ambayo imebadilisha maisha ya vijana wengi hapa jiji la Arusha.”

error: Content is protected !!