BoT yaanzisha vita na wanaotumia noti vibaya

HomeKitaifa

BoT yaanzisha vita na wanaotumia noti vibaya

Gavana wa Benki kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Florens Luoga ametangaza kuchukua hatua kwa watu wanaotumia vibaya noti katika shughuli za kijamii ikiwemo sherehe kwa kuzirusha sakafuni, kuweka katika mwili uliolowa jasho na kuzitumia kama mapambo.

Taarifa ya BoT imeeleza kuwa
“Watu wamekuwa na tabia ya kutunza wahusika wa matukio kwa kuwarushia noti zinazoanguka sakafuni na muda mwingine kukanyagwa, kuzivingilisha katika maumbo mbalimbali, kuitumia kama mapambo, kuweka katika mwili uliolowa jasho na matukio yanayofanana na hayo”

“Kwa tarifa hii BoT itaanza kuchukua hatua dhidi ya wale wote watakaohusika na vitendo vya matumizi mabaya ya noti ya Tanzania kwa njia yoyote ile ikiwemo kuweka fedha sakafuni na sehemu yoyote ambayo sio nadhifu,” alisema Luoga.

Aidha alisema vitendo hivyo vinachangia kutweza fedha na kusababisha uchakavu hivyo kuongezea Serikali gharama ya kuchapisha fedha zingine huku akiwataka washiriki katika matukio ambayo yanahusisha matumizi ya fedha kuandaa vyombo maalumu vya kuweka fedha hizo badala ya kufanya vitendo ambavyo havikubaliki.

 

error: Content is protected !!