Bwawa la Nyerere lazidi kujaa

HomeKitaifa

Bwawa la Nyerere lazidi kujaa

Ujazo wa maji katika bwawa la kufua ueme la Julius Nyerere (JNHPP) linalotarajiwa kujaa ndani ya miezi 18 hadi jana ulifika mita 108.31 kutoka usawa wa bahari.

Ujazaji wa maji katika bwawa hilo linalotarajiwa kuzalisha megawati 2,115 za umeme likiwa na uwezo wa kuhifadhi lita bilioni 32 ulianza Desemba 22 mwaka jana.

Meneja Mawasiliano wa Uhusiano wa Wadau wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Elihuruma Ngowi alisema bwawa linaendelea kujaa kwa kasi kwa sababu yamejikusanya kwenye eneo dogo.

“Muda wa kujaa bado ni uleule yaani misimu miwili ya mvua. Mita zinaonekana ziko juu kwa sababu maji yamejaa sehemu moja, lakini yakianza kusambaa maeneo mengine, zitakuwa zinakwenda taratibu,” alisema Ngowi.

Wakati maji ya masika ya mwaka jana na mwakani yakiendelea kujaa, alisema shughuli nyingine za ujenzi zinaendelea.

“Ujenzi hautosimama, mwenendo wa bwawa kujaa maji ni mzuri,” alisema Ngowi. 

error: Content is protected !!