CAG abaini madudu Uwanja wa Ndege Chato

HomeKitaifa

CAG abaini madudu Uwanja wa Ndege Chato

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere amesema gharama za ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Chato mkoani Geita zilizidi bajeti iliyotengwa kwa sababu ulifanyika bila upembuzi yakinifu.

CAG alisema kutofanyika kwa upembuzi yakinifu kunaongeza hatari kwa Seriklai kuwekeza katika mradi usio na tija na uwezekano wa kuwapo gharama zisizodhibitiwa na ongezeko la muda katika utekelezaji wake.

“Mpatio yangu yalibaini Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) hawakufanya upembuzi yakinifu kabla ya kuanz aujenzi,” amesema Kichere.

CAG Kichere amesema Sh3.62 bilioni za mradi huo zilitolewa kwenye miradi mingine kwa matarajio kwamba zingerejeshwa baada ya Hazina kutoa fedha zake, jambo ambalo halikutekelezwa kwa wakati hivyo kusimamisha miradi mingine iiliyopangwa.

error: Content is protected !!