CAG ageukia fedha za UVIKO-19

HomeKitaifa

CAG ageukia fedha za UVIKO-19

Mdhibiti  na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere, amesema ofisi yake imeanza kufanya ukaguzi maalumu wa matumizi ya fedha za UVIKO-19 zilizopelekwa kwenye halmashauri nchini. Hayo aliyabainisha jana wakati wa kikao cha baraza la wafanyakazi wa ofisi hiyo kilichofanyika jijini Dodoma.

“Tunampongeza Mheshimiwa Rais Samia kwa namna alivyotoa maelekezo ya matumizi ya fedha za kukabiliana na janga la UVIKO-19. Ninampongeza Rais kwa namna alivyotoa maelekezo ya matumizi ya fedha za kukabiliana na UVIKO-19, hususani afya, elimu, maji na hatua anazochukua za kudhibiti matumizi ya fedha hizo”. alisema Kichere

CAG Charles Kichere amesema ofisi yake inaunga mkono jitihada za Rais Samia, hivyo haina budi ofisi yake kutelekeleza jukumu lake la kikatiba kwa kuanza ukaguzi kwenye halmashauri zilizopata fedha hizo.

“Mheshimiwa mgeni rasmi (Katibu Mkuu Kiongozi) nikuhakikishie kwamba tutafanya ukaguzi wa fedha hizo zote za UVIKO-19 zilizotolewa na kila senti ya fedha hizo itakaguliwa na taarifa itatolewa, ili kuhakisha fedha hizo zimetumika kulingana na maelekezo, taratibu, sheria na miongozo ya matumizi ya fedha za umma”. alisema Kichere

 

error: Content is protected !!