Deni la serikali hadi Aprili 2023, lilikuwa shilingi bilioni 79,100.19 sawa na ongezeko la asilimia 13.9 ikilinganishwa na Shilingi bilioni 69,440.01 kwa kipindi kama hicho mwaka 2022.
Ongezeko la deni limetokana na : kupokewa kwa fedha za mikopo kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli, viwanja vya ndege, umeme, elimu na afya.
Tathmini iliyofanyika inaonyesha kuwa deni la serikali ni himilivu na viashiria vya deni viko ndani ya wigo unaokubalika kimataifa katika kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu.