Dkt. Samia aagiza fedha za sherehe ya kuadhimisha 9 Desemba zikarabati miundombinu iliyoharibiwa Oktoba 29

HomeKitaifa

Dkt. Samia aagiza fedha za sherehe ya kuadhimisha 9 Desemba zikarabati miundombinu iliyoharibiwa Oktoba 29

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan ameagiza fedha za sherehe zilizopangwa kuadhimisha Desemba 9, 2025 zitumike kukarabati na kuboresha miundombinu iliyoharibiwa na vurugu za Oktoba 29.

Kauli ya Dkt Samia imetolewa leo Jumatano na Waziri Mkuu, Dkt Mwigulu Nchemba kwa niaba yake wakati akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam, baada ya kufanya ziara ya kukagua miundombinu ya umma na binafsi iliyoaharibiwa na vurugu za Oktoba 29 na 30, 2025.

Miongoni mwa maeneo yaliyoathiriwa ni pamoja na miundombinu ya mabasi na vituo vya mwendokasi, zahanati vituo vya polisi vilivyopo maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam,”

” Nitoe kauli ya mwisho mheshimiwa Rais ( Dkt Samia) ameelekeza Desemba 9 hakutakuwa na sherehe za kuadhimisha hiyo Desemba 9, gharama za fedha zilizopangwa kutumika ameelekeza kutengeneza miundombinu hii iliyoharibika,”

“Kuanzia leo sekta zinahusika mkae, mratibu fedha zile zote zilizotakiwa ziende kwenye sherehe mheshimiwa Rais ( Dkt Samia ) ameelekeza ziende kurekebisha miundombinu iliyoharibika,” amesema Dk Mwigulu.

Dkt Mwigulu ameitaka Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, pamoja na sekta zingine zinazohusika kuratibu mchakato ili maelekezo ya Rais Dkt Samia yatekelezwe ili kurejesha miundombinu hiyo.

error: Content is protected !!