Donge nono kwa atakayefichua wezi wa mita

HomeKitaifa

Donge nono kwa atakayefichua wezi wa mita

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), imetangaza donge nono la Sh 500,000 kwa mtu atakayefichua wezi na waharibifu wa mita za maji kwenye mji huo.

Sebastian Warioba ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Duwasa alitoa taarifa hiyo iliyobainisha kuwa hatua hiyo imetokana na kukithiri wizi na uharibifu wa mita za maji vinavyosababisha hasara na usumbufu kwa mamlaka na wateja.

“Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma inatangaza donge nono la Shilingi 500,000 kwa yeyote atakayetoa taarifa sahihi itakayowezesha kukamatwa kwa wezi na waharibifu wa mita za maji… Taarifa hiyo itolewe kwa kuwasiliana na Mkurugenzi Mtendaji au kwa simu namba 0756162432,” alisema Warioba.

Aidha, Warioba alieleza namna ambvyo taarifa hiyo inatakiwa kutolewa ili kuweza kuwakamata wezi hao wa mita za maji jijini Dodoma.

“Pia taarifa ibainishe mita zinazoibiwa zinapelekwa wapi na kwa malengo gani na zile mita zinazoharibiwa zinaharibiwa kwa malengo gani,” alisema.

error: Content is protected !!