Kwanza kabisa tambua kwamba kirusi hicho hakizalishwi maabara kama watu wengi wanavyozusha kwenye mitandao ya kijamii na mitaani. Ukweli ni kwamba huu ni muendelezo wa kusambaa wa Corona hivyo kuufanya ugonjwa huo kujinyumbulisha virusi vipya.
Ukweli kuhusu kirusi cha Corona aina ya ‘OMICRON’
- Kadri ugonjwa wa Uviko- 19 unavyosambaa ndivyo unavyounda aina mpya ya kirusi ikiwemo ‘OMICRON’
- Siyo kweli kwamba kirusi hicho kimetengenezwa maabara, tofauti na upotoshaji unaofanywa mtandaoni.
- Kirusi cha ‘OMICRON’ kinauwezo mkubwa wa kujibadilisha , hivyo wanasayansi wanaendelea kubaini madhara yake na chanjo inayoweza kukidhibiti.
Wakati tukisubiri majibu ya wanasayansi tuendelee:
- Kuvaa barakoa
- Kunawa mikono
- Kupata chanjo
- Kuepuka mikusanyiko
Njia nzuri zaidi za kujilinda na ugonjwa huu ni kupata chanjo na kuendelea kuchukua tahadhari zingine.