Fahamu kuhusu kimbunga ‘Freddy’

HomeKimataifa

Fahamu kuhusu kimbunga ‘Freddy’

 Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa ufafanuzi kuhusu uwepo wa  kimbunga ‘Freddy’ kilichopo kusini magharibi mwa bahari ya Hindi karibu na pwani ya Madagascar, kilichotarajiwa kuikumba pwani ya afrika mashariki mwanzoni mwa wiki hii.

Kwa mujibu wa ufafanuzi huo uliotolewa jana February 20,2023, TMA imesema kimbunga hicho hakina madhara ya moja kwa moja  kwenye maeneno mengi yaliyopo nchini tofauti na upotoshaji unaoendelea kwenye kwenye mitandao ya kijamii.

“TMA inaendelea kufuatilia kwa kina mwenendo wa kimbunga hiki na itatoa taarifa punde tu kutakapokuwa na haja ya kufanya hivyo”, inasema taarifa hiyo.

Kwa takribani  kipindi  cha wiki moja iliyopita kulizuka taarifa ya ujio wa kimbunga hicho ikiripotiwa na vyombo vya habari mbalimbali vya kitaifa na mamlaka za hali ya hewa za kimataifa ikiwemo Taasisi ya Hali ya Hewa Duniani (WMO).

Hii si mara ya kwanza kwa tahadhari za vimbunga kutangazwa ukanda wa Afrika Mashariki na nchini Tanzania,.

 Mwaka 2021 mamlaka hiyo ilitangaza ujio wa kimbunga ‘Jobo’   kilichotarajiwa kuathiri maeneo ya pwani ya Tanzania mnamo April 25,2 2021.

Kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuibuka kwa upepo kinzani kwenye ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi kimbunga hicho kilizidiwa nguvu na kushindwa kuathiri maeneo yalyliyokusudiwa.

error: Content is protected !!