Watano kati ya 19 waliokuwa wabunge Chadema wateuliwa CCM Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imewateua miongoni mwa waliokuwa wabunge 19 wa Chadema kuwania ubunge. Wabunge hao baada ya Bunge la 12 kuvunjwa walihamia CCM na kujitosa kwenye majimbo.
Walioteuliwa na majimbo yao ni Esther Matiko (Tarime Mjini), Ester Bulaya (Bunda Mjini), Hawa Mwaifunga (Tabora Mjini), Kunti Majala (Chemba) na Jesca Kishoa (Iramba Mashariki.)
Majina hayo yametangazwa leo Jumamosi Agosti 23, 2025 na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla wakati akitangaza majina ya wagombea watakaopeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba mwaka huu.