Fahamu zaidi kuhusu mkutano atakaohutubia Rais Samia Marekani

HomeKitaifa

Fahamu zaidi kuhusu mkutano atakaohutubia Rais Samia Marekani

Rais Samia Suluhu Hassan ameondoka nchini na kwenda Marekani kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kidiplomasia kubwa ikiwa ni mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Tumekuwekea baaadhi ya dondoo muhimu kuhusu mkutano huo.

Baraza Kuu la Umoja ni nini?

Ni chombo kikubwa zaidi cha Umoja wa Mataifa kinachoundwa na nchi zote wanachama (nchi 193). Ndicho chombo kinachofanya maamuzi ya msingi ya umoja huo ikiwemo kuteua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (kwa kushirikiana na Baraza la Usalama), kupitisha bajeti za Umoja wa Mataifa na kuchagua wanachama wa mpito (non-permanent members) wa Baraza la Usalama.

Mkutano wa mwaka huu ni kwa waliochanjwa tu

Kwa kawaida Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hukutana kila mwaka kati ya mwezi Septemba na Desemba ili kujadili na kupitisha masuala mbalimbali yanayoihusu dunia. Mwaka 2020, mkutano wa Baraza ulifanyika kwa njia ya mtandao kutokana na hatari ya maambukizi ya ‘COVID-19’ hivyo mwaka huu viongozi watakaohudhuria mkutano huo, wamepewa sharti la kwamba lazima wawe na uthibitisho kwamba wamepata chanjo ya Corona.

Rais Samia kuhutubia Baraza 

Viongozi wa nchi zitakazohudhuria mkutano huo, watapata nafasi ya kuhutubia. Rais Samia Suluhu yeye atatoa hotuba yake siku ya Alhamisi, Septemba 23,2021.

Wengine watakaohutubia siku hiyo ni pamoja na viongozi kutoka Afrika Kusini, Guyana, Botswana, Cuba, Angola,  Namibia, Morocco,  Cameroon, Zimbabwe,  Liberia,  Burundi, Benin, Bolivia, Rwanda na Uganda,

error: Content is protected !!