Faida 5 za kujamiiana asubuhi

HomeElimu

Faida 5 za kujamiiana asubuhi

Huwenda umeshawahi kusikia kuhusu umuhimu wa kushiriki tendo la ndoa asubuhi na ukashangaa lakini ni kweli kuna faida za kufanya tendo hilo kwa afya yako na wataalamu wanasema ni moja wapo ya matibabu.

ClickHabri tunakusogezea baadhi ya faida za kushiriki tendo la ndoa asubuhi kutokana na utafiti uliofanywa na Dr.Sudeshna.

Huimarisha kumbukumbu

Ngono asubuhi inaweza kusaidia ubongo wako kuwa na nguvu siku nzima na pia kukusaidia kuwa na kumbukumbu hivyo unashauriwa kushiriki kial upatapo nafasi.

Ni mazoezi tosha

Unapofanya ngono asubuhi ni kama unafanya mazoezi kwani kuna kilo na mafuta yanapungua pindi unaposhiriki. 

Huongeza kinga ya mwili

Ni vizuri kushiriki tendo la ndoa asubuhi kwani huongeza kinga za mwili sababu wakati wa tendo hilo mwili unazalisha antibodi ya IgA inayosaidia katika ulinzi wa mwili dhidi ya magonjwa.

Hukupa nguvu ya kazi

Baada ya tendo la ndoa mwili huwa mwepesi na tayari kwa ajili ya kufanya kazi na ndio maana mnashauri kabla hujaenda kazini ili usiende kuharibu kazi na kuonekana mvivu ni bora ukajamiiana.

Hizo ni baadhi za faida ya kushiriki tendo la ndoa asubuhi lakini unashauri uhakikishe kwamba hamtumii muda mrefu kama ambavyo mngeweza kufanya usiku.

error: Content is protected !!