Furahia wikiendi na filamu ya ‘The girl allergic to Wi-Fi’

HomeBurudani

Furahia wikiendi na filamu ya ‘The girl allergic to Wi-Fi’

Huwenda ukawa umewahi kusikia magonjwa mengi lakini je, umeshawahi kusikia ugonjwa wa mtu kutoruhusiwa kuwa karibu na sehemu yenye mtandao au kutumia mitandao? Najua unashangaa inawezekanaje.

Basi filamu hii inayokwenda kwa jina la ‘A Girl Allergic to Wi-Fi” inamuhusu binti Norma ambaye yeye maisha yake yote ni mtandaoni lakini anakuja kujua baadae kwamba anaumwa ugonjwa huo kitaalamu unafahamika kama “Electromagnetic Hypersensitivity Syndrome” yani haruhusiwi kuwa karibu kabisa na mtandao kwani kwakufanya hivyo damu umtoka pua na kuzimia.

A Girl Allergic to Wi-Fi

Njia pekee yakupona ni kwenda sehemu ambayo hakuna kabisa mtandao, hivyo basi Norma anasafiri mpaka kijijini kwa bibi yake na kuacha kila kitu mjini pamoja na mpenzi wake Leo ambaye alishaanza kuonyesha kutomjali Norma tangu alipoanza kuumwa.

Baada ya kufika kijijini mdogo wake Leo, Aries anaanza kuonyesha upendo wa hali ya juu kwa Norma kuliko hata kaka yake ambaye amemlia buyu Norma na hana muda wakwenda kumsalimia kijijini jambo linalompa wasiwasi mrembo huyo.

Muda mwingine katika maisha unapopoteza kila kitu ndipo unapata mapenzi ya dhati, Je, ni nini kitatokea baada ya Norma kwenda Kijijini na Leo kuanza kumlia buyu huku Aries akianza kuonyesha mapenzi kwa shemeji yake?

error: Content is protected !!