Njia bora 4 za kufanya meno yang’ae

HomeElimu

Njia bora 4 za kufanya meno yang’ae

Kila mtu anapenda kuwa na meno masafi meupe yanayong’aa ili pindi akicheka, akitabasamu au hata kuongea basi yaonekane vizuri, lakini wengi wameshindwa kujua namna yakupata muonekano huo kwani njia nyingi ni kwa kutumia dawa zenye kemikali.

ClickHabari kwa kuwa tunajali afya yako, basi tunakusogezea njia rahisi 4 ambazo uhitaji kutumia kemikali kusafisha meno.

Piga mswaki kila siku

Hakikisha unapiga mswaki kila baada ya kula na kabla hujalala, wakati unapiga mswaki weka dawa ya meno kinywani kwa dakika kadhaa kabla yakuitema. Ukifanya hivyo kila siku hakika meno yako yatapendeza

Sukutua na mafuta

Tumia mafuta ya asili, mfano mafuta ya nazi kusukutua mdomoni hii itakusaidia kuondoa harufu mbaya kinywani na pia kuacha meno katika hali nzuri.

Tumia mkaa

Jaribu kutengeneza dawa yako ya meno, chukua mkaa, usage kisha lowesha meno yako alafu upake mkaa na kuanza kusugua. Fanya hivyo mara kwa mara ili meno yaweze kung’aa.

Tumia vijiti vya mwarobaini

Unaweza pia kukata kijiti kwenye mti wa mwarobaini na kukigeuza kuwa mswaki na kuutumia kila siku. Baada ya muda utaanza kuona mabadiliko kwenye kinywa chako.

error: Content is protected !!