Kauli ya Rais Samia kuhusu mauaji ya Mtwara

HomeKitaifa

Kauli ya Rais Samia kuhusu mauaji ya Mtwara

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri Mkuu Kasim Majaliwa kuunda kamati itakayochunguza mauaji yaliyofanywa na Jeshi la Polisi kwa kusema haiwezekani mauaji yafanyike na jeshi hilo na kujifanyie uchunguzi.

“Haiwezekani Jeshi lifanye mauaji Jeshi lichunguze lenyewe, ndugu zangu wananchi na watanzania nimemuelekeza Waziri Mkuu aunde kamati nyengine iende ikafanye uchunguzi wa mauaji yaliyofanywa na jeshi la polisi alafu watuletee taarifa,” alisema.

“Lakini wakati huo huo Mheshimiwa Waziri nataka jeshi lako lijitafakari waone kama kinachotokea ndio misingi ya jeshi la polisi au vyenginevyo, kwahiyo tutasuburi ndugu wananchi taarifa ya kamati huru itakayoundwa na Waziri Mkuu ituletee taarifa tulinganishe na ile ya jeshi la polisi na tuone taarifa mbili zinasemaje tuchukue hatua muafaka,” alisema Rais Samia Suluhu.

Amesema hayo akiwa safarini kuelekea Musoma kwenye maadhimisho ya miaka 45 CCM.

error: Content is protected !!