Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) imeitenga nchi ya Guinea baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika ndani ya taifa hilo.
Maamuzi hayo yameambatana na agizo linaloagiza nchi ya Guinea kurejesha kwenye utawala wa katiba na sheria.
Kikosi maalum chini ya Kanali Mamady Doumbouya kiliongoza mapinduzi hayo na kumweka kizuizini aliyekuwa Rais la Taifa hilo, Alpha Konde.
Viongozi kutoka mataifa 15 ya ECOWAS walifanya kikao kwa njia ya mtandao kujadili hatma ya taifa la Guinea na baada ya kikao walikubaliana kulitenga mara moja. ECOWAS imelitaka jeshi la Guinea kumwachia Conde na kuwakamata wote waliofanikisha mapinduzi na kupelekwa mbele ya sheria.
ECOWAS ilikuchukua uamuzi kama huo mwaka jana wakati wa mapinduzi ya nchi Mali. ECOWAS waliweka vikwazo vya kiuchumi kwa Mali hadi pale jeshi liliporejesha utawala wa kisheria nchini humo.