Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dr. Doroth Gwajima ametoa taarifa kwa umma kufuatia tukio la udhalilishaji wa binti mwanafunzi lililotokea hivi karibuni, na ambalo lilihusisha mabinti wanafunzi wa vyuo vikuu.
Akirejea taarifa yake ya awali iliyotolewa tarehe 20 Aprili, 2025, Waziri ameeleza kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa kina na kuwahoji wote wanaohusishwa na tukio hilo kwa mujibu wa sheria za nchi.
Aidha, Waziri amegusia maswali yanayoibuliwa na wananchi kuhusu kutokukamatwa kwa mtu aliyejulikana kwa jina la Mwijaku, ambaye ametajwa na kuonekana katika video zinazohusiana na tukio hilo. Amesisitiza kuwa Mwijaku naye atahojiwa na vyombo vya dola kwa mujibu wa sheria, na baada ya hapo, Wizara itachukua hatua stahiki kuhusu nafasi yake na athari zake katika jamii, hasa katika masuala ya maadili.
Waziri ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa watulivu, kufuatilia taarifa rasmi kutoka Jeshi la Polisi, na kuendeleza ushirikiano na Serikali katika kuhakikisha haki, maadili na ustawi wa jamii vinalindwa.
TAARIFA KWA UMMA
KUH; MABINTI WANAFUNZI WA VYUO VIKUU WALIOMDHALILISHA BINTI MWENZAO.
Dar es Salaam, 23 Aprili, 2025.
Ndugu Wananchi, rejeeni taarifa yangu kwa umma ya tarehe 20 Aprili, 2025 kuhusu mada tajwa hapo juu. Jeshi letu la Polisi linaendelea kutimiza wajibu wake wa… pic.twitter.com/EDON8k00bh
— Dr. Dorothy Gwajima (@Dr_DGwajima) April 23, 2025