Harmonize amwomba Kajala amrudie

HomeBurudani

Harmonize amwomba Kajala amrudie

Msanii na mmiliki wa Konde Gang, Harmonize amlilia mpenzi wake wa zamani Kajala Masanja jukwaani akipokea tuzo mbili usiku wa Tuzo za Muziki Tanzania.

Akitoa neno mara baada ya kupokea tuzo ya Wimbo Bora Shirikishi wa Afrika 2021 (Attitude) Harmonize amemmwagia sifa Kemkem Kajala.

“Nataka kusema tena hii ni kwaajili ya malkia, ninaposema malkia namaanisha Frida Kajala Masanja. Hii ni kwaajili yako mamaa. Siku zote umekua ukinihimiza kufanya kazi na hatimaye tumeweza,” amesema Harmonize.

Akiendelea kuomba msamaha kwa yaliyotokea Harmonize akatumka nafasi hiyo kumwomba Kajala aweke kando yaliyopita ili waweze kuganga yajayo.

“Ninaomba urudi tuishi maisha tuliyokuwa tumepanga. Nakupenda sana, naomba nirudi na nitasema hili kwa sauti, samahani nilikukosea.”

Tuzo nyingine alizopokea Harmonize ni pamoja na Mwanamuziki Bora wa Kiume wa mwaka na Mtumbuizaji Bora wa Kiume wa Mwaka

error: Content is protected !!