Masoud Kipanya aja na gari la kuchaji

HomeKitaifa

Masoud Kipanya aja na gari la kuchaji

Mtangazaji na mchora katuni maarufu nchini Tanzania, Masoud Kipanya kupitia kampuni yake ya Kaypee Motors amezindua gari ndogo ya mizigo inayotumia umeme leo Aprili 4, 2022 huku akieleza kwamba gari hiyo inafaa zaidi kwa kubebea mizigo.

Masoud amesema alianza kutengeneza gari hilo mwaka 2020 akiwa na timu ya watu wachache walioungana kulikamilisha gari hilo.

Akiongelea lengo la kutengeneza gari hilo ni kuionyesha Afrika kwamba hakuna kinachoshindikana na kuiondoa ile dhana ya kwamba yapo mambo yanayowezwa na wenye ngozi nyeupe tu.

error: Content is protected !!