Wanaume: fahamu M3 hizi

HomeElimu

Wanaume: fahamu M3 hizi

Kwa mwanaume yoyote yule ambaye yupo kwenye mahusiano au ana mpango wakuanzisha mahusiano basi ni lazima akawa anazifahamu vyema M3 ambazo zitamsaidia kwenye safari yake ya mapenzi.

Inafahamika kwamba msichan yoyote yule anapenda kuona mwanaume wake anampenda kwa kumfanyia mambo kadha wa kadha, hivyo basi ili uweze kuwa bora kwenye mahusiano yako basi zingatia ‘M’3 hizi.

Mlinde

Kila msichana anapenda kuona mwanaume wake anamlinda kwa namna yoyote hili hasa mbele za watu, kwa kufanya hivyo utamfanya akupende zaidi na kukuamini.

Mfano mzuri ni jinsi muigizaji Will Smith alivyoweza kusimama kwa niaba ya mke wake usiku wa tuzo za Oscar kitendo kilichofanya dunia itambue jinsi gani anampenda mama wa watoto wake.

Pia hata katika kumshauri kwenye maamuzi ambayo unaweza kuona kuna shida inaweza kutokea.

Mhudumie

Hakikisha una muhudumia mwanamke wako na pale ambapo huna basi kuwa muwazi na umuambie ukweli, na ndio maana wanaume wanashauriwa kama wanaona mwanamke fulani hatoweza kumuhudumia ni vyema ukaachana naye kuliko ulazimishe mahusiano ambayo hutoweza kuhudumia hapo mbeleni.

Unapo muhudumia yeye basi atapata uhakika kwamba unaweza hata kuhudumia familia hapo mbeleni.

Msimamie na Mpende

Kama mwanaume ni wajibu wako kusimama kwa niaba ya mwanamke wako na pia kuhakikisha watu wanatambua kwamba wewe ni mchumba wa mtu fulani.

Mfano mnaweza kwenda kwa marafiki na wewe ukamtambulisha mchumba wako kwa jina lake “Mambo zenu wanangu, huyu ni Zaituni”, hapo umetenda kosa kwani mwanamke atahisi haumpendi na ndio maana hutaki watu wajue mahusiano yenu.

Unachotakiwa kufanya ni kumtambulisha vizuri watu wajue kwamba ni mchumba wako na mpo kwenye mahusianao.

error: Content is protected !!