Hatimaye mkataba wa TPA na TICTS wafika tamati

HomeKitaifa

Hatimaye mkataba wa TPA na TICTS wafika tamati

Hatimaye kilio cha wadau wa bandari kimesikika baada ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kusitisha mkataba wake na Kampuni Binafsi ya Kimataifa ya Kuhudumia Makontena Tanzania (TICTS) mwaka huu.

Hii ni baada ya TICTS kuhudumia katika Bandari ya Dar es Salaam kwa miaka 22 bila mafanikio huku wadau wa bandari wakiomba mkataba usitishwe kwani TICTS imeshindwa kufikia malengo na kusababisha hasara.

TICTS imehudumu katika bandari ya Dar es Salaam kwa miaka 22 sasa tangu mwaka 2000 kwa mara ya kwanza iliposaini kutoa huduma ya makontena.

Kuhusu nia ya menejimenti ya TPA kusitisha mkataba huo na TICTS, kwa kile ilichofafanua mazungumzo baina ya pande hizo mbili hayakufanikiwa, kutokana na kutokubaliana katika vigezo vya ibara ndogo ya 2.2.1 ya mkataba huo.

Aidha, TPA inayoongozwa na Plasduce Mbossa imeiomba baraka bodi ili waweze kuiandikia barua kampuni hiyo kutohuisha mkataba huo, na tayari wamejipanga kusimamia wenyewe shughuli zilizokuwa zikifanywa na TICTS.

“Sina shaka hata kidogo kwamba bodi itakubali ombi hili. Na tayari tumejipanga kuhakikisha tunasimamia wenyewe wakati tunatafuta mtu mwingine ambaye atakuwa na uwezo mkubwa zaidi,” alisema kigogo mmoja.

 

error: Content is protected !!