Baada ya uchunguzi kufanywa kuhusu tukio la video fupi iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari ikiwahusisha watumishi wawili, Bi. Rose Shirima ( Muuguzi Mkunga) na Bw. Getogo James Chuchu (Mteknolojia wa Maabara), wafanyakazi wa Zahanati ya Ishihimulwa iliyoko Halmashauri ya Uyui, Mkoani Tabora ambao walikuwa wakijibizana kuhusu matumizi ya vifaa vya kupimia Malaria (mRDT), mambo yafuatayo yamebainika.
a. Kuna mahusiano yasiyoridhisha baina ya watumizi mahala pa kazi.
b. Matumizi ya lugha isiyo na staha mahali pa kazi,
c. Usimamizi wa kituo usioridhisha.
d. Watumishi wanne wa Zahanati ya Ishihimulwa wamekutwa na tuhuma za kujibu
e. Hakuna mteja (mgonjwa) aliyepimwa Malaria kwa kutumia vitendanishi vilivyoisha muda wake wa matumizi licha ya uwepo wa vitendanishi vilivyoisha muda wake wa matumizi tangu wmezi Agosti 2022.
f. Ilibainika kuwa kituo hicho kina vitendanishi ambavyo vitaisha muda wake ifikapo wmezi Aprili na Desema 2023.
HATUA ZILIZOCHUKULIWA
a. Kusimashiwa kazi kwa Bi. Rose Shirima kwa tuhuma za matumizi ya lugha isiyo na staha mahali pa kazi na Bw. James Chuchu amekutwa tuhuma ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii na kuleta taharuki katika jamii.
b. Sambamba na hilo Bi. Rose Shirima na Bw. James Chuchu wamefikishwa kwenye mabaraza ya kitaaluma kujibu tuhuma walizokutwa nazo.
c. Kamati za Afya za Wilaya na Mkoa zimeelekezwa kuimarisha usimamaizi wa karibu katika vituo vya kutolea huduma na kutatua changamoto zinazojitokeza kwa wakati.