Historia ya Tanzania kuwa somo mashuleni

HomeKitaifa

Historia ya Tanzania kuwa somo mashuleni

Historia ya Tanzania itaanza kufundishwa mwakani kama somo katika shule za msingi na sekondari kama alivyoagiza Rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli kamba lianze kufundishwa kama somo la kujitegemea.

Taarifa hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omari Kipanga wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Chumbuni, Ussi Salum Pongeza (CCM).

Pongeza alitaka kujua ni lini somo hilo la historia litaanza kufundishwa kama Rais John Magufuli alivyoagiza lianze kufundishwa kama somo linalojitegemea shuleni.

 

error: Content is protected !!