Auawa kwa kuchomwa kisu baada ya kukataa kuolewa

HomeKitaifa

Auawa kwa kuchomwa kisu baada ya kukataa kuolewa

Mauaji ya mwanafunzi mmoja wakike aliyefahamika kwa jina la Nayera Ashraf nchini Egypt yamezua mjadala mkubwa baada ya kuhusishwa kwa wivu wa mapenzi na unyanyasaji wa kijinsia.

Nayera alipigwa na kuchomwa kisu majira ya mchana nje ya chuo chake na mwanaume mmoja ambaye alikua anamsubua mwanamke huyo kwa miezi kadhaa baada ya kutomkubalia ombi lake la kumuoa.

Kabla ya kifo chake, Nayera aliwahi kwenda kutoa taarifa polisi na amri ikatolewa kwa mwanaume huyo kukaa mbali naye kitendo kilichomfanya azidi kumsumbua mwanadada huyo na kumlazimisha kumuoa.

Matukio ya unyanyasaji zaidi ya 813 dhidi ya wanawake yameripotiwa nchini Egypt kwa mwaka 2021.

error: Content is protected !!