Mahakama yamtoza mtoto wa Simbachawene faini laki 2

HomeKimataifa

Mahakama yamtoza mtoto wa Simbachawene faini laki 2

Mfanyabiashara, James Simbachawene (24) ambaye ni mtoto wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), George Simbachawene, amehukumiwa kulipa faini ya Sh250, 000 na kufungiwa leseni yake ya udereva kwa miezi sita baada ya kukiri makosa matatu.

Mshtakiwa huyo amefikishwa mahakamani hapo leo Jumatano Agosti 24, 2022 jioni na kusomewa mashtaka yake na wakili wa Serikali, Daisy Makakala, mbele ya Hakimu Mkazi Aron Lyamuya.

Mashtaka hayo ni pamoja na kuendesha gari kwa hatari, kuendesha gari akiwa amelewa na kuendesha gari bila kuwa na bima.

SOURCE: MWANANCHI

error: Content is protected !!