Karani wa Sensa ajifungua Bunda

HomeKitaifa

Karani wa Sensa ajifungua Bunda

Wakati Sensa ya Watu na Makazi ikiendelea vizuri katika Wilaya za Bunda na Rorya mkoani Mara, mmoja wa makarani wa sensa hiyo wilayani Bunda amejifungua mtoto usiku wa kuamkia leo.

Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Joshua Nassary amesema mmoja kati ya makarani zaidi ya 1, 000 amejifungua mtoto usiku wa kuamkia leo, hivyo idadi ya watu waliohesabiwa wilayani humo, imeongezeka.

Amesema mpaka wakati akizungumza, tukio hilo lilikuwa changamoto pekee ingawa kwa upande mwingine ni baraka inayowaongezea sababu za kushukuru Mungu.

“Alipojifungua, kwa kuwa tunao makarani wa akiba, mmoja akachukua nafasi, kazi zinaendelea,” amesema Nassary.

Amewaondoa wasiwasi wanaompigia simu wakisema hawajahesabiwa, kwamba hakuna mwana Bunda atakayeachwa bila kuhesabiwa, waendelee kutoa ushirikiano kama wanavyofanya tangu kazi hiyo ilipoanza.

error: Content is protected !!