Huduma za mahakama kupatikana kwenye simu

HomeUncategorized

Huduma za mahakama kupatikana kwenye simu

Mhimili wa Mahakama nchini Tanzania umeanzisha utoaji mrejesho kuhusu ubora wa huduma za mahakama kupitia simu janja

Mtendaji Mkuu wa Mahakama Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel, amesema huduma za mahakama sasa zinapatikana kupitia mfumo wa kielektroniki wa kutoa mrejesho kuhusu ubora wa huduma za mahakama kupitia simu ya kiganjani au tovuti ya mahakama (www.judiciary.go.tz).

Mfumo huo ni rahisi kuutumia na kwamba taarifa zitakazopokelewa zitatumika kuboresha huduma za Kimahakama na sio vinginevyo.

Jinsi ya kutoa taarifa kupitia simu yako ya kiganjani
i. Bofya ‘Google Playstore’ tafuta Judiciary Mobile Tz’
ii. Pakua na kufungua, bofya kitufe cha ‘Mrejesho’
iii. Pakua na kuanza kutumia.

Mahakama imesema kwa wale ambao wanatumia simu za kawaida wanaweza kutuma ujumbe mfupi (sms) au kupiga simu kwenye dawati la mrejesho ambalo linafanya kazi masaa 24. Namba 0752500400.

error: Content is protected !!