Watu 443 wamefariki dunia kufuatia mafuriko na mmomonyoko wa ardhi KwaZulu-Natal, nchini Afrika Kusini huku wengine 63 wakiendelea kutafutwa wasionekane.
Mafuriko hayo yamewaacha mamia bila makazi, maji safi ya kunywa wala umeme.
“Kila kitu ni ukumbusho unaoumiza wa kile tulichopoteza, na kutoweza kumpata (Bongeka) ni jambo la kuumiza kwa sababu hatuwezi kuhuzunika au kupona. Katika hatua hii tunaachwa ukijihisi watupu,” amesema Lethiwe Sibiya (33) mama wa mtoto Bongeka aliyepotea baada ya ukuta wa chumba walicholala kuangushwa na mafuriko aliiambia Reuters.
Hali hiyo imepelekea Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini kusitisha safari yake ya kikazi Saudi Arabia katika kipindi hiki kigumu kwa nchi hiyo.