Jibu la Ferrari chanzo cha kuzaliwa Lamborghini

HomeMakala

Jibu la Ferrari chanzo cha kuzaliwa Lamborghini

Katika maisha si kila mtu anaweza kupokea ushauri na kuufanyia kazi, au kukosolewa akaridhika na kuyafanyia kazi makosa yake. Ni ngumu kujihariri mapungufu yetu, na ni rahisi kwa wengine kuona mapungufu yetu, lakini pindi mtu anapofuatwa na kuelezwa mapungufu yake aidhia juu yake au kitu anachofanya, ni wachache wenye uungwana wa kupokea kwa tabasamu, lakini wengi huchukizwa.

1963 Ferruccio Lamborghini akiwa mtengenezaji wa matrekta, hakufurahishwa na gari aina ya Ferrari aliyokuwa akitumia, kwakuwa aligundua shida katika mfumo wake wa breki. Kwakuwa alimjua mmiliki na mtengenezaji wa magari hayo, aliamua kufunga kumfuata Enzo Ferrari na kumueleza shida iliyopo kwenye magari yake na kumpa ushauri namna ya kuboresha mfumo wa breki zake.

Enzo Ferrari hakumpa jibu zuri Ferruccio zaidi ya kumwambia kuwa yeye ni mkulima aendelee kutengeneza matrekta huku yeye akitengeneza magari, jibu hili halikuwa zuri kabisa kwa Lamborghini hivyo akaweka nia ya kuanza kutengeneza magari kwa sababu alikua anapenda masuala ya injini, hivyo akaondoka na wazo la kuanzisha kampuni yake ya Lamborghini.

Baada ya miezi minne Ferruccio alitangaza rasmi gari aina ya Lamborghini 350 GT huku watu wakishangaa imewezekana vipi gari kukamilika kwa muda mchache?, kumbe wafanyakazi waliounda gari hiyo walitoka kwenye kampuni ya Ferrari, na hii ni baada ya kutimuliwa na Enzo kwa sababu walimwambia ukweli kuhusu mke wake kujipa madaraka na kufanya maamuzi ya ovyo kwenye kiwanda hicho.

Tangu hapo Ferruccio alianza kutengeneza magari mengi na kampuni kuwa kubwa duniani , Lamborghini ni kati ya magari yanayopendwa sana hasa na watu maarufu kama wasanii wanaodiriki mpaka kuyataja kwenye nyimbo zao na mpaka sasa Ferrari na Lamborghini ni kampuni zenye ushindani mkubwa sana.

Hivyo basi katika maisha usije ukafikiri kwamba kila mtu anaweza kukubaliana na mawazo yako, unachotakiwa kufanya ni tumia ujuzi huo kutengeneza kitu bora zaidi kwani unaweza ukawa Ferrari kumbe ndoto zako ni kufika mbele zaidi kama Lamborghini.

error: Content is protected !!