Juhudi za Rais Samia zimepandisha uwezo wa Tanzania kukopesheka

HomeKitaifa

Juhudi za Rais Samia zimepandisha uwezo wa Tanzania kukopesheka

Kutokana na hatua zilizochukuliwa na Rais Samia Suluhu, viwango vya Tanzania vimepanda kwenye tathmini ya kukopesheka na kuvutia uwekezaji kutoka nje iliyofanywa na Moody’s.

Katika taarifa iliyotolewa Oktoba 7, na taasisi ya Moody’s Investors Service imesema vihatarishi vya kisiasa vimepungua nchini kutokana na mkakati wa Serikali kufufua uchumi kwa kuihusisha jumuiya ya kimataifa hivyo kuingizwa daraja B2 la kukopesheka na taasisi za fedha hata jumuiya za kimataifa.

“Juhudi za serikali kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji hasa kwenye sekta ya madini zinatoa matumaini ya kukuza uchumi kwa kiasi kikubwa na kuongeza ushindani wa Tanzania kimataifa.

“Kupungua kwa vihatarishi vya kisiasa kunatoa fursa ya kuboresha ukuaji wa uchumi kuweza kukabiliana na athari za majanga ya kidunia zitokanazo na uvamizi wa Russia nchini Ukraine.” inasema tathmini hiyo.

Hata hivyo, ripoti hiyo imesema licha ya ukuaji mzuri wa uchumi wa Tanzania unaotegema rasiliamli za sekta tofauti hivyo kuweza kuhimili changamoto zinazosababishwa na majanga ya kidunia, pato la kila mwananchi bado ni dogo na kuna udhaifu wa kitaasisi unaodhoofisha uwezo wa kiuchumi.

 

 

 

error: Content is protected !!