Jumuiya ya wakala wa forodha yampongeza Rais Samia kuruhusu uwekezaji wa DP World

HomeKitaifa

Jumuiya ya wakala wa forodha yampongeza Rais Samia kuruhusu uwekezaji wa DP World

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wakala wa Forodha Zanzibar na Mjumbe wa JWT, Omary Hussein, amesema mkataba ambao Rais Samia ameusaini ni wa kufungua milango ya kibiashara na kiuchumi iliyokuwa imekwama.

Ameyasema hayo jana visiwani Pemba, wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa, suala la bandari kilikuwa kilio cha muda mrefu cha wafanyabishara wengi nchini

Amesema kwa upande wa Zanzibar watanufaika na kusainiwa kwa mkataba huo kwasababu walikuwa wakitumia zaidi bandari ya Mombasa kushusha mizigo yao na kwa maboresho hayo watatumia bandari ya Dar es Salaam.

“Tumpongeze Rais Samia kwa maono yake makubwa yanayofungua uchumi wa Taifa na kurahisisha shughuli za kibiashara nchini kupitia TPA na kurahisisha shughuli za uwekezaji nchini, tunamshukuru na kumpongeza sana,” alisema Omary.

error: Content is protected !!