Kama umetumia mswaki mmoja kwa muda huu, uko hatarini!

HomeElimu

Kama umetumia mswaki mmoja kwa muda huu, uko hatarini!

Inawezekana watu wengi wakawa wanapiga mswaki kama utamaduni tu, lakini wasiwe wanaelewa zaidi faida, hasara au hata tahadhari za kuchukua kwenye kutekeleza kitendo hicho.

Je, unafahamu kwamba kuna bakteria na vijidudu vingi zaidi ya milioni 10 vinavyoishi kwenye mswaki wako? Takwimu zisikuogopeshe, kwa watafiti wanasema kwamba bakteria hawa waishio ndani ya vinywa vyetu na miswaki yetu haviwafanyi watu waugue.

Hapa ndipo unapaswa kujua sasa namna sahihi ya kusafisha kinywa chako Karibu.

1. Usipige mswaki chini ya dakika mbili
Wataalamu wa Afya ya kinywa wanashauri kwamba kupiga mswaki kwa usahihi, ni zaidi ya dakika mbili, chini hapo kuna hatari ya kinywa chako kutotakata vizuri na kupelekea madhara kwenye kinywa. Hivyo basi, kwa uhakika zaidi, mtu anapaswa kupiga mswaki zaidi ya dakika mbili.

2. Uache mswaki wako ukiwa msafi na mkavu
Baada ya kuswaka, hakikisha unaosha mswaki wako vizuri, tena kwa maji tiririka. Baada ya hapo ukung’ute hadi maji yaisha kwenye  mswaki, kuna hatari sana wadudu wakazaliana zaidi kwenye mswaki kama utauacha umeloana. Kukausha mswaki itakusaidi kuukuta ukiwa mkavu ukitaka kupiga tena.

3. Uhifadhi kwa kuusimamisha
Kusimamisha mswaki ni muhimu sana baada ya kuutumia. Usimamishe kwenye kikombe maalumu au kifaa maalumu cha kuhifadhia miswaki. Hii itafanya mswaki wako kukauka haraka na kupata hewa safi ambayo itasaidia kuua vijidudu.

4. Weka mswaki wako mbali na shimo la choo
Hasa hivi vyoo vya kisasa ambavyo unaweza kujikidhi haya zako wakati umeketi na ‘kuflash’ baada ya kumaliza, ndio hatari zaidi. Kwani wakati unaflash choo, kuna hewa inatoa chooni ambayo hubeba bakteria na kutoka nje. Hatudhani kama ungependa hewa hii ikutane na mswaki ambao unauingiza mdomoni kila siku kusafisha kinywa chako. Wataalamu wanashauri mswaki ukae angalua futi tatu kutoka kwenye tundu la choo.

5. Usitumie mswaki zaidi ya miezi mitatu
Taasisi ya afya ya kinywa Marekani inasema kuwa mswaki unapaswa kutumika kwa miezi mitatu tu. Hapa kuna jambo la kuzingatia, kujua mswaki umeisha muda au la, ni vyema kuangalia hali ya mswaki wako, angalia ile ‘brush’ kama imeanza kuchoka au kuisha, hapo utajua hali ya mswaki wako.

Si vyema sana kufuata kalenda kwani unaweza kuutupa mswaki  wako angali mzima bado. Kila mtu ana matumizi yake ya nguvu kwenye kupiga mswaki, hivyo kuisha kwa mswaki kutategemeana na watu tofauti.

error: Content is protected !!