Kenya: Shule za fungwa kupisha maandamano

HomeKimataifa

Kenya: Shule za fungwa kupisha maandamano

Serikali nchini Kenya imetoa agizo la kufungwa kwa shule zote za msingi na sekondari za mchana jijini Nairobi na Mombasa kabla ya maandamano ya upinzani yaliyopangwa kufanyika na muungano wa Azimio kuanzia Jumatano wiki hii.

Katika taarifa ya pamoja iliyosainiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Profesa Kithure Kindiki na mwenzake wa Elimu Ezekiel Machogu, mawaziri hao wawili walibainisha kuwa ripoti za ujasusi zenye kuaminika zimebainisha mipango ya kundi la watu wahalifu kushambulia shule maalum katika kaunti hizo mbili ili ‘kutawanya hofu na kuleta vurugu kwa umma’ wakati wa maandamano.

“Serikali imepokea taarifa ya ujasusi wa usalama inayoaminika kuwa watu wahalifu wamepanga kushiriki katika mapigano yenye silaha na vyombo vya usalama karibu na shule zilizochaguliwa ndani ya Jiji la Nairobi na Mombasa,” inasomeka taarifa hiyo iliyoonekana na Citizen Digital.

“Kama tahadhari ya kuhakikisha usalama wa watoto wa shule, imeamuliwa kuwa shule zote za msingi na sekondari za mchana ndani ya jiji la Nairobi na Mombasa ZITABAKI kufungwa kesho.”

Wizara ya Elimu itatangaza tarehe ya kuanza tena kwa masomo katika shule hizo baada ya tathmini ya hali ya usalama siku ya Jumatano.

Taarifa ya mawaziri hao wawili ilifuatiwa na taarifa kutoka kwa Mkuu wa Polisi Japhet Koome ambayo iliyatangaza maandamano ya Azimio yaliyopangwa kuwa ni kinyume cha sheria.

Kulingana na Koome, kundi linaloongozwa na Raila Odinga halikuwasilisha taarifa rasmi kwa polisi kuhusu mikusanyiko iliyopangwa hadi Jumanne jioni.

Hivyo, aliwaonya Wakenya dhidi ya kushiriki katika maandamano hayo akisema kuwa polisi watashughulika ipasavyo na waandamanaji.

error: Content is protected !!