Khaby wa Tiktok apewa rasmi uraia wa Italia

HomeKimataifa

Khaby wa Tiktok apewa rasmi uraia wa Italia

Mchekeshaji Khaby Lame, anayeongoza kwa kufuatiliwa zaidi kwenye mtandao wa TikTok duniani, amepewa uraia wa Italia katika hafla iliyofanyika katika mji wa Kaskazini wa Chivasso karibu na mji wa Turin alikokulia.

Khaby ni mzaliwa wa Senegala lakini aliishi Italia tangu akiwa na umri wa mwaka mmoja, alianza kupata umaarufu baada ya kupoteza kazi aliyokuwa akiifanya kwenye moja wapo ya kiwanda kutokana na mlipuko wa Covid-19.

Aliamua kuanza kutengeneza maudhui mbalimbali kwenye mtandao wa Tiktok yaliyomfanya kuwa maarufu na kuweza kupata ubalozi wa vitu na pia kukutana na watu maarufu kama wachezaji mpira na waigizaji.

 

error: Content is protected !!