Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesema kuanzia leo kutakuwa na operesheni maalumu ya kuwasaka vijana, maarufu Panya Road wanaofanya matukio ya kihalifu.
Amesema operesheni hiyo itaanza leo usiku na hakuna atakayesalimika.
“Kuanzia leo, baada ya tamko langu, hakuna ‘Panya Road’ atasalimika katika mkoa wa Dar,
“Opersheni inayoanza usiku wa leo si salama kwa ‘Panya Road,”.
Ameongeza “Niwasihi wazazi kwamba operesheni hii haitowaacha watoto wao wahalifu, kama mzazi ulizoea kupata zawadi kwa mtoto, TV bila kujua kipato chake, asikudanganye ‘amebeti’, kawatafuteni watoto wenu kwenye vituo vya Polisi kuanzia kesho” amesema Makalla.
Aidha, Mhe. Makalla amesema kila Wilaya kwa mikoa ya Kipolisi, kutoa taarifa za kila siku za ‘Operesheni ondoa ‘Panya Road’ na kudhibiti uhalifu katika mkoa wa Dar es Salaam kila siku, toeni taarifa tusipotoa taarifa watazitoa taarifa mbaya”
Ameyasema hayo siku moja baada ya kundi hilo la uvamizi kuvamia na kujeruhi watu 19 Kunduchi mkoani humo.
Hivi karibuni, Rais Samia Suluhu Hassan alilitaka kundi hilo kusitisha mara moja vitendo hivyo.