Kinara mishahara EAC

HomeKitaifa

Kinara mishahara EAC

Marais wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wameboresha maslahi ya watumishi kwa kuongeza kima cha chini cha mishahara kwa viango tofauti.

Viongozi hao wa kuu kutoka Tanzania, Kenya, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), walitangaza uamuzi huo kwa nyakati tofauti katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) mwaka huu na wengine kuahidi kulifanyika kazi jambo hilo.

TANZANIA

Katika maadhimisho yaliyofanyika kitaifa jijini Dodoma, Rais Samia Suluhu Hassan alitimiza ahadi yake ya kupandisha mishahara ya watumishi katika Mwaka wa Fedha wa 2022/2023.

“Ulezi wa mama unaendelea, yale tuliyofanya mwaka huu ya kupunguza kodi na kuona hiki, tutaendelea kuyafanya. Lakini pamoja na hayo ‘lile jambo letu’ lipo,” alisema Rais Samia.

Rais Samia Suluhu aliweka wazi kwamba mchakato unaendelea wa kufanya mahesabu ili mishahara hiyo iweze kupandishwa na leo Mei 14 ametimiza ahadi hiyo kwa kuongeza ikiwemo kima cha chini kwa watumishi wa umma kwa 23.3%.

Ongezeko hili linaifanya Tanzania kushika nafasi ya pili kwa nchi za Afrika Mashariki zilizoongeza mishahara mikubwa kwa watumishi wake wa umma.

DRC

Jamhuri ya Demokrasia ya Congo inashika nafasi ya kwanza kwa nchi za Afrika Mashariki zilizoongeza mishahara kwa watumishi wake wa umma.

Naibu Waziri Mkuu, Jean-Pierre Lihau anayehusika na masuala ya utumishi wa umaa, alitoa tangazo Aprili 29,2022 siku mbili kabla ya Mei Mosi kwamba serikali imeongeza kima cha chini cha mishahara kwa watumishi kwa asilimia 30.

UGANDA

Rais Yoweri Museveni aliwaambia wafanyakazi katika uwanja wa Kololo jijini Kampala kuwa anakubaliana na maombi ya Chama cha Wafanyakazi ch uganda (NOTU), kupandisha kima cha chini ili kuwa na ulinganifu wa mishahara lakini utekelezaji utafanyika kwa kuzingatia vipaumbele vya taifa. 

Alisema kwa sasa kipaumbele kikubwa cha serikali yake ni watumishi wa kada ya sayansi ambao taifa linawahitaji kwa kiwango kikubwa hivyo baada ya hao kada zingine zitafuata.

KENYA

Rais Uhuru Kenyatta, alitangaza nyongeza ya asilimia12 kwa mishahara ya kima cha chini kwa watumishi katika sekta zote. Rais Uhuru alitoa tangazo hilo juzi katika Uwanja wa Nyayo mjini Nairobi, wakati wa sherehe za Mei Mosi.

error: Content is protected !!