Kuna haja ya ujenzi wa barabara nane

HomeKitaifa

Kuna haja ya ujenzi wa barabara nane

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana amesema sasa ni wakati mwafaka kwa serikali kujenga barabara ya njia nane kwa Dar es Salaam-Tunduma ili iwe na njia nne kwa kila upande.

Amesema lengo ni kuharakisha usafiri na usafirishaji ikiwamo kutatua kero ya foleni ambazo huchelewesha huduma mbalimbali.

Kinana ametoa kauli hiyo jana Julai 29, 2022 wakati akizungumza na wana CCM katika kikao cha ndani kilichofanyika ndani ukumbi wa Benjamin Mkapa jijini Mbeya, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi na kuimarisha uhai wa Chama.

Katika taarifa yake Kinana amesema ni vizuri kama Taifa kutumia gharama kubwa kuja na dira ya kujenga miundombinu ya uhakika itakayodumu zaidi ya miaka 50 itakayondoa kero na kuleta ustawi wa maisha ya watu.

“Imeamuliwa kujenga barabara nne hapa Mbeya na fedha zimeshatolewa na zabuni ya kuwapata wakandarasi imeshatangazwa kwa ajili ya ujezi, kazi iliyopo ni kuharakisha wakandarasi wapatikane na ujenzi uanze haraka ili ikifika mwaka 2025 barabara ikamilike,” amesema na kuongeza,

“Lakini jana kila wakati nikisafiri kutoka Tunduma kuja hapa Mbeya mjini mawazo yangu yananielekeza sasa Tanzania imefika wakati wa kuwa na barabara nne nne kutoka Dar es Salaam hadi Tunduma tusifanye vipande vipande ndugu wabunge.” alisema Kinana.

error: Content is protected !!